name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
Kama umewahi kushangazwa na matokeo mazuri ya mwanafunzi katika mtihani wa kuvuka ngazi moja kwenda | Kama umewahi kushangazwa na matokeo mazuri ya mwanafunzi katika mtihani wa kuvuka ngazi moja kwenda nyingine ya elimu, ilhali hakuwa na historia ya umahiri darasani Mwananchi inakufichulia siri iliyojificha nyuma ya muujiza huo.
Si bahati kama wengi wanavyodhani, yapo mambo mengine yanayochagiza ufaulu wa wanafunzi kat... |
Serikali imeagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kunusuru kupanda kwa b | Serikali imeagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kunusuru kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo nchini.
Hatua hiyo ya Serikali imechagizwa na ongezeko la bei na uhaba wa bidhaa hiyo katika Mikoa mbalimbali.
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la ghafla la bei ya sukari. Mathalan kat... |
Rais Samia Suluhu Hassan amesema athari za vita na Ugonjwa wa Uviko-19, ndizo zilizochagiza mdororo | Rais Samia Suluhu Hassan amesema athari za vita na Ugonjwa wa Uviko-19, ndizo zilizochagiza mdororo wa kiuchumi duniani kwenye sekta ya uzalishaji na hatimaye kuathiri upatikanaji wa Dola za Marekani.
Rais Samia ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Desemba 31, 2023 alipotoa salamu za mwaka mpya 2024 kwa Wa... |
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatakubali kuzibwa au kuongozwa na itikadi za kisiasa k | Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatakubali kuzibwa au kuongozwa na itikadi za kisiasa katika kazi ya Mungu.
Mbowe alitoa kauli hiyo mkoani Kilimanjaro jana, alipoongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa kanisa la Bethel, Usharika wa Nshara wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambalo yeye ni mu... |
Saa 22 ziligeuka shubiri kwa wakazi wa Mtaa wa Mwanamtoti Darajani, Mbagala jijini Dar es Salaam, ku | Saa 22 ziligeuka shubiri kwa wakazi wa Mtaa wa Mwanamtoti Darajani, Mbagala jijini Dar es Salaam, kutokana na eneo hilo kubainika kitu kilichodaiwa kuwa bomu.
Hali hiyo ilizua hofu kwa wakazi hao, kutokana na kile walichoeleza imechukua muda mrefu kwa Jeshi la Polisi kuliondoa bomu hilo, licha ya kuarifiwa mapema.
Kuli... |
Kukithiri kwa matukio ya vifo vya watu wa familia moja kutokana na ajali, kunatajwa kusababisha maba | Kukithiri kwa matukio ya vifo vya watu wa familia moja kutokana na ajali, kunatajwa kusababisha mabadiliko ya mtindo wa kusafiri kwa wanafamilia katika siku za hivi karibuni.
Mabadiliko hayo, yanahusisha kuwagawa ndugu katika usafiri tofauti badala ya ilivyozoeleka kwamba kwa safari moja familia hutumia usafiri wa pamo... |
Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Wanawake Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Em | Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Wanawake Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Emmanuel Silanga kuhusu eneo la uchimbaji madini mkoani Simiyu, umefika mwisho.
Hatua ya kufika mwisho kwa mgogoro huo, imetokana na Serikali ya mkoa wa Simiyu kuingilia kati na kuamua uendeshaji wa leseni hiyo ufanywe kwa... |
Kama kwako Krismas ilikwenda sawa ni jambo la kumshukuru Mungu, maana wapo iliyowaacha na huzuni, ik | Kama kwako Krismas ilikwenda sawa ni jambo la kumshukuru Mungu, maana wapo iliyowaacha na huzuni, ikiwemo familia ya Isaya Ndindindi, iliyopoteza vijana wawili katika fukwe za Bahari ya Hindi.
Vijana hao, Elisha Isaya (18) na Richard Robert (14) walipoteza maisha walipojaribu kuvuka katika moja ya mikondo ya bahari hiy... |
Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Emmanuel Si | Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Emmanuel Silanga kuhusu eneo la uchimbaji madini mkoani Simiyu, umefika Mwisho.
Hatua ya kufika Mwisho kwa mgogoro huo, imetokana na Serikali mkoani humo kuingilia kati na kuamua umiliki wa mgodi huo uwe kwa ubia kati ya Tawoma na ... |
Joto la Uchaguzi Mkuu katika taifa la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, linaendelea kupanda, huku Watan | Joto la Uchaguzi Mkuu katika taifa la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, linaendelea kupanda, huku Watanzania wakisisitiza umuhimu wa amani ili kulinda uhusiano wa kibiashara na kindugu baina ya wananchi wa mataifa hayo.
Kupanda kwa joto hilo la uchaguzi wa Desemba 20, mwaka huu kunatokana na ukweli kwamba, zimesalia siku... |
Matumaini ya utekelezwaji wa mabadiliko ya kikokotoo kwa watumishi wastaafu wa Jeshi la Polisi, yapo | Matumaini ya utekelezwaji wa mabadiliko ya kikokotoo kwa watumishi wastaafu wa Jeshi la Polisi, yapo mikononi mwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni aliyesema kinachofanywa naye sasa ni utekelezaji.
Hata hivyo, Masauni hakuweka wazi juu ya hatua hizo za utekelezaji zilizofikiwa, kwa kile alichokisisitiza, ... |
Hatimaye Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na | Hatimaye Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.
Wito huo uliotolewa jana na Mahakama ya Wilaya ya Babati, umekuja baada ya Wakili wa kujitegemea, Pet... |
Katika kukabiliana na migogoro ya kikodi iliyopo baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na walipa | Katika kukabiliana na migogoro ya kikodi iliyopo baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na walipakodi, Serikali imeanzisha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania (TOST).
Katika taasisi hiyo, mlalamikaji hatalazimika kuwa na uwakilishi wa mwanasheria ili awasilishe malalamiko, badala yake ana... |
Licha ya Serikali ya Tanzania kuweka wazi juu ya sababu ya kutoonekana hadharani kwa Makamu wake wa | Licha ya Serikali ya Tanzania kuweka wazi juu ya sababu ya kutoonekana hadharani kwa Makamu wake wa Rais, Dk Philip Mpango bado ukimya wa kiongozi huyo umeendelea kuibua mashaka kwa baadhi ya Watanzania.
Hoja kuhusu ukimya wa Dk Mpango, imeibuliwa na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii, wakihoji yu wapi Makamu huyo... |
Ni usiku wa vilio na hasara kwa wafanyabiashara, ndiyo maneno mafupi unayoweza kutumia kuelezea uhal | Ni usiku wa vilio na hasara kwa wafanyabiashara, ndiyo maneno mafupi unayoweza kutumia kuelezea uhalisia wa matukio matatu ya ajali ya moto yaliyotokea katika maeneo tofauti katika Jiji la Dar es Salaam.
Matukio hayo yamehusisha kuungua moto kwa maduka ya bidhaa mbalimbali eneo la Mwenge, kuungua kwa maduka ya samani z... |
Serikali imeshauriwa kuwa na sera itakayowashawishi mawakili wake kuendelea kufanya kazi nayo, badal | Serikali imeshauriwa kuwa na sera itakayowashawishi mawakili wake kuendelea kufanya kazi nayo, badala ya kutafuta fursa katika kampuni binafsi.
Imeelezwa hatua hiyo itawezesha mawakili nguli kuendelea kufanya kazi na Serikali na hivyo, kuwezesha kushinda kesi za madai hasa za kimataifa ambazo Tanzania haina historia n... |
Taarifa za hadi jana za madhara ya maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang, zinaonyesha wanawake ndiy | Taarifa za hadi jana za madhara ya maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang, zinaonyesha wanawake ndiyo walioathirika zaidi ukilinganisha na wanaume.
Katika tukio hilo lililoanza kutokea juzi, waliopoteza maisha ni 63 kati yao wanawake ni 40 sawa na asilimia 67 na wanaume 23 sawa na asilimia 33.
Kwa upande wa majeruhi ni... |
Simanzi zaidi imeikumba familia ya Magreth Daraja, aliyepoteza ndugu watano baada ya kufunikwa na to | Simanzi zaidi imeikumba familia ya Magreth Daraja, aliyepoteza ndugu watano baada ya kufunikwa na tope hilo katika maeneo mbalimbali.
Kulingana na Magreth ndugu aliowapoteza ni mjukuu wake, dada yake, kaka zake wawili waliofunikwa na tope wakiwa ndani ya nyumba, huku mama yake akisombwa hadi mtoni na kufariki.
“Hapa na... |
Madhara ya maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, yamesababisha kusombwa kwa n | Madhara ya maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, yamesababisha kusombwa kwa nguzo 60 za laini ndogo ya umeme, huku nguzo za laini kubwa tano zikianguka.
Kusombwa na kuanguka kwa nguzo hizo, kumesababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya Wilaya hiyo yenye jumla ya wateja 13... |
Tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa inayoishia mwaka 2025, inaonyesha wastani wa pato la mtanza | Tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa inayoishia mwaka 2025, inaonyesha wastani wa pato la mtanzania mmoja umeongezeka kutoka Sh322,597 mwaka 2000 hadi Sh2.88 milioni Desemba 2022.
Ongezeko hilo, linatajwa kuwa sehemu ya mafanikio ya utekelezaji wa dira hiyo ya kwanza, inayotarajiwa kukoma miaka miwili ijayo na hivy... |
Kama ni umri wa binadamu sasa amefikia utu uzima, hivi ndivyo unavyoweza kuielezea miaka 36 ya Chama | Kama ni umri wa binadamu sasa amefikia utu uzima, hivi ndivyo unavyoweza kuielezea miaka 36 ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa).
Tamwa iliyozaliwa miaka 36 iliyopita, kwa mujibu wa waasisi wake, chimbuko la kuanzishwa kwake ni juhudi za kusaka nguvu ya sauti ya wanawake katika vyumba vya habari.
Histori... |
Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na uny | Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na unyanyasaji wa kingono katika vyombo vya habari.
Hayo ni kulingana na utafiti wa hali ya usalama wa wanahabari wanawake katika vyumba vya habari uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika vyombo vy... |
Wingi wa watu, fursa na huduma ni miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wengi nchini Tanzania, ku | Wingi wa watu, fursa na huduma ni miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wengi nchini Tanzania, kufungasha virago kutoka vijijini na kwenda kuanza maisha katika maeneo ya Miji.
Kulingana na mtazamo wa vijana wengi wa Tanzania, ni rahisi kufanikiwa unapokuwa mjini kwa kuwa kuna kazi nyingi za kufanya, tofauti na kiji... |
Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na uj | Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na ujuzi na maarifa muhimu ili kujenga ustawi wa karne ya 21.
Kwa kutambua hitaji hilo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua mpango wa kuanzisha klabu za kidigitali, unaolenga kukuza ujuzi wa kidijitali na ubunif... |
Wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ikitabiri kuendelea kwa mvua nchini, wataalamu mbalimbali wames | Wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ikitabiri kuendelea kwa mvua nchini, wataalamu mbalimbali wameshauri mbinu za kuepuka madhara yatakayotokana na hali hiyo, ikiwemo kuwataka wananchi wapunguze safari zisizo za lazima.
Wamekwenda mbali zaidi wakipendekeza mbinu kama ilivyofanyika wakati wa Uviko-19 zitumike, ikiwemo ... |
Matumaini ya wadau wa siasa juu ya kukoma kwa utaratibu wa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia ucha | Matumaini ya wadau wa siasa juu ya kukoma kwa utaratibu wa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia uchaguzi yanaendelea kuyeyuka, baada ya Serikali kuwasilisha bungeni muswada unaopigia msumari uhalali wa jambo hilo.
Kwa mujibu wa wadau hao, wakurugenzi kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Rais kuwa na mamla... |
Safari ya kuisaka suluhu ya mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, imeonekana kuwa m | Safari ya kuisaka suluhu ya mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, imeonekana kuwa mfupa mgumu uliowashinda viongozi wengi, baada ya ahadi na hatua zilizowahi kutangazwa nao kukosa matokeo chanya.
Historia ya janga la mafuriko katika eneo hilo ina miongo kadhaa, huku vifo na familia kuachwa bila makazi ... |
Mjue Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wa kipekee ba | Mjue Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wa kipekee barani Afrika, anayewakilisha mafanikio na mwendelezo wa siasa za kidemokrasia Tanzania. Akichukua nafasi ya uongozi wakati mgumu baada ya kifo cha ghafla cha Rais John Pombe Magufuli mwaka 2021, Samia aliweka historia kwa... |
Wakati wananchi wakilalamikia kuongezeka kwa makato ya kodi ya majengo kuanzia Julai 1 mwaka huu, Sh | Wakati wananchi wakilalamikia kuongezeka kwa makato ya kodi ya majengo kuanzia Julai 1 mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema ongezeko hilo ni malipo ya deni walilopaswa kukatwa Julai mwaka jana.
Kwa mujibu wa shirika hilo, kodi ya jengo kwa nyumba za kawaida imesalia kuwa Sh1,500 kwa mwezi na ghorof... |
Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Yusuph Manji amezikwa jana Florida nchini Marekani, akiacha histori | Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Yusuph Manji amezikwa jana Florida nchini Marekani, akiacha historia ya kuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa waliowahi kutokea nchini.
Heshima na jina lake, lisingekuwa kitu kipya katika masikio ya Watanzania wengi nyakati hizo, hiyo ilitokana na utajiri wake, kadhalika kujihusisha kwa... |
Vilio vya watu kutoweka na kutekwa vimeendelea kushika kasi nchini, huku wadau wakiinyooshea kidole | Vilio vya watu kutoweka na kutekwa vimeendelea kushika kasi nchini, huku wadau wakiinyooshea kidole Serikali kwa madai kuwa kuna viashiria vya kuhusika kwake.
Kwa mujibu wa wadau hao wa kada mbalimbali, kinachoashiria ushiriki wa Serikali ni madai kuwa, watekaji wengi wanapokwenda kumchukua mtu hujitambulisha kuwa ni ... |
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema atakuwa tay | Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema atakuwa tayari kushiriki mdahalo wowote nchini unaolenga kujadili kwa hoja kuhusu utendaji wa Serikali na mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli kama hiyo imewahi kutolewa na mtangulizi wa Makalla katika nafasi hiyo, Paul M... |
Kwa kumbukumbu zangu mjadala kuhusu vazi la taifa umekuwepo tangu enzi za Serikali ya awamu ya nne, | Kwa kumbukumbu zangu mjadala kuhusu vazi la taifa umekuwepo tangu enzi za Serikali ya awamu ya nne, ni kumbukumbu zangu, sijui ilikuwaje kabla ya wakati huo.
Wakati huo wizara iliyokuwa na dhamana hiyo iliitwa, Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na waziri wake alikuwa Emmanuel Nchimbi, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu ... |
Hatua ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kufanya mabadiliko katika sekretarieti ya CCM, | Hatua ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kufanya mabadiliko katika sekretarieti ya CCM, imehusishwa na maandalizi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.
Mambo mengine yanayotajwa kuchagiza mabadiliko hayo kwa mujibu wa wanazuoni mbalimbali ni kukisafisha chama hic... |
Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kufikia Desemba mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ahakikishe | Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kufikia Desemba mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ahakikishe mifumo yote ndani ya Serikali inasomana.
Hii si mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa nchi kutoa maelekezo hayo, aliwahi kufanya hivyo Juni 9, mwaka jana katika Baraza la Biashara Dar es Salaam, akitaka kuharakishwa kwa mabor... |
Taasisi za umma na binafsi zinazohusika na shughuli ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi z | Taasisi za umma na binafsi zinazohusika na shughuli ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi za watu, zimetakiwa kuhakikisha zifanyanya kazi hiyo zikiwa na vibali stahiki.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Aprili 3, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Emmanuel Mt... |
Huenda mrithi wa Paul Makonda katika nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na | Huenda mrithi wa Paul Makonda katika nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, asitofautiane sana na mwanasiasa huyo, kwa maana ya mtindo wa uongozi.
Mtindo wa Makonda katika miezi michache ya uongozi wake ndani ya CCM, zimeshuhudiwa amsha amsha zilizokiwe hai chama hicho nap engine kuvut... |
Katika siku za hivi karibuni, hautalazimika tena kutembea na nauli mkononi kwa ajili ya kupanda dala | Katika siku za hivi karibuni, hautalazimika tena kutembea na nauli mkononi kwa ajili ya kupanda daladala, baada ya mpango wa Serikali kutumia tiketi mtandao katika usafiri huo.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zinatarajia kuanzisha mfumo wa matumizi ... |
Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaketi leo, katika kikao chake cha kikatiba amba | Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaketi leo, katika kikao chake cha kikatiba ambacho aghalabu hufanyika mara mbili kila mwaka na inapolazimika hufanyika zaidi.
Kinaweza kuwa miongoni mwa vikao vilivyobeba shauku kubwa ya wana-CCM na wadau wa siasa, kutokana na mazingira yaliyopo wakati wa kufanyika ... |
Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema iwapo kitendo cha kushambuliwa k | Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema iwapo kitendo cha kushambuliwa kwake kwa risasi kimesababishwa na hatua yake ya kuwatetea wafugaji, akisisitiza ataendelea kufanya hivyo.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo aliweka wazi kuwa tukio la kushambuliwa kwake halihusiani na utetezi wake wa ardhi kw... |
Bunge la bajeti linaanza leo huku Watanzania wakitaka wabunge kujielekeza katika mambo yanayojikita | Bunge la bajeti linaanza leo huku Watanzania wakitaka wabunge kujielekeza katika mambo yanayojikita kwenye kupunguza umasikini wa watu ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi.
Machi 11, 2024 akiwasilisha ukomo wa bajeti na mapendekezo ya mpango wa Taifa wa maendeleo wa mwaka 2024/25 Waziri wa FedhaDk Mwigulu Nchemba alisema ... |
Nani kurithi mikoba ya Paul Makonda na Anamringi Macha? swali hili ndilo linalofanya macho na masiki | Nani kurithi mikoba ya Paul Makonda na Anamringi Macha? swali hili ndilo linalofanya macho na masikio ya Wana-CCM na Watanzania kuelekezwa katika vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) vinavyotarajiwa kuanza kesho.
Vikao hivyo vya kamati kuu na Halmashauri kuu, kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha ndani ya cham... |
“Nikiwa na umri wa miaka 19, baba yangu alinilazimisha niolewe, sikuwa namjua mwanaume, hakutaka kum | “Nikiwa na umri wa miaka 19, baba yangu alinilazimisha niolewe, sikuwa namjua mwanaume, hakutaka kumtambulisha na hata nimuone,” Ni maneno ya binti Ruwaida Ally (21), akisimulia namna alivyowekwa katikati ya mtego wa ndoa, ambayo hakuwa na mpango nayo.
Ruwaida alijikuta katika mtego huo baada ya kuhitimu kidato cha nn... |
Kama umewahi kula msoto kitaa kwa miaka kadhaa baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu, bila shaka u | Kama umewahi kula msoto kitaa kwa miaka kadhaa baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu, bila shaka utaelewa ni magumu gani ameyapitia kijana John Alexander (29).
Alexander ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa uunganishaji umeme wa majumbani katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida, ni kie... |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa am | Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ametoa miezi saba kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), kuhakikisha inapatikana kampuni binafsi itakayotoa huduma ya usafiri.
Iwapo hilo halitatekelezwa hadi Oktoba mwaka huu, Mchengerwa amewataka Wakurugenzi Dart ... |
Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa | Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya nishati.
Rais Samia aliianza safari ya urais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, Hayati John Magufuli, aliyefariki Mac... |
Ilianza siku, wiki, mwezi, mwaka na hatimaye miaka mitatu ndani ya wadhifa wa urais, ndivyo unavyowe | Ilianza siku, wiki, mwezi, mwaka na hatimaye miaka mitatu ndani ya wadhifa wa urais, ndivyo unavyoweza kuichambua safari ya Rais Samia Suluhu Hassan kama mkuu wa nchi.
Rais Samia aliapishwa kuwa Rais, Machi 19, mwaka 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, John Magufuli, aliyefariki Machi 17, mwaka huo.
Mata... |
Wakati leo ukitimia mwaka wa tatu tangu alipofariki Rais wa awamu ya tano, John Magufuli, familia ya | Wakati leo ukitimia mwaka wa tatu tangu alipofariki Rais wa awamu ya tano, John Magufuli, familia yake imeweka wazi namna kifo cha kiongozi huyo kilivyoonyesha sura halisi za binadamu.
Kulingana na wanafamilia ya Hayati Magufuli, enzi za uhai wa kiongozi huyo, familia hiyo ilidhani ina marafiki na watu wengi wanaoipen... |
Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020/25, imeielekeza Serikali kufanikisha upati | Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020/25, imeielekeza Serikali kufanikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 95 kwa maeneo ya mijini, lakini asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini.
Hata hivyo, hotuba ya makadirio ya fedha, mapato na matumizi ya Wizara ya Maji katika mwaka wa fedha 2023/24, ime... |
Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa | Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya nishati.
Rais Samia aliianza safari ya urais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, Hayati John Magufuli, aliyefariki Mac... |
Udhibiti wa mianya ya wizi wa makusanyo na kutegua kitendawili cha mkwamo wa vipuli vya mabasi katik | Udhibiti wa mianya ya wizi wa makusanyo na kutegua kitendawili cha mkwamo wa vipuli vya mabasi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni sehemu ya mzigo unaomkabili Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart), Waziri Kindamba.
Mengine yanayosubiri utendaji wake ni kuboresha huduma za usafiri... |
Licha ya kupatikana kwa uongozi mpya wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) na Wakala wake (Da | Licha ya kupatikana kwa uongozi mpya wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) na Wakala wake (Dart), wadau wameonyesha mashaka, wakieleza uwezekano wa utenguzi wa mabosi hao kuendelea kutokana na uhalisia wa huduma.
Kwa mujibu wa wadau wa usafirishaji, kuendelea kwa utenguzi na uteuzi mpya wa mabosi wa Dart na Uda... |
Kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kimefuta matumaini ya wananchi katika kiji | Kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kimefuta matumaini ya wananchi katika kijiji cha Binga wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani kupata Shule ya Sekondari na Hospitali.
Kufutika kwa matumaini hayo, kunatokana na kile walichoeleza, Hayati Mwinyi enzi za uhai wake aliwaahidi kuwajengea shule hiyo ... |
Bohari ya Dawa (Msd), imesema kuna haja ya kuwa na akiba ya mifuko ya kuhifadhia damu itakayodumu kw | Bohari ya Dawa (Msd), imesema kuna haja ya kuwa na akiba ya mifuko ya kuhifadhia damu itakayodumu kwa kipindi cha kuanzia miezi mitano hadi tisa, ili kuepuka kuadimika kwake.
Kauli hiyo ya MSD inakuja katika kipindi ambacho, akiba ya mifuko hiyo kwa sasa ni miezi mitatu, jambo linalopaswa kuongezeka kutokana na ongeze... |
Miaka mitatu si safari nyepesi, aghalabu inahusisha milima na mabonde, katika hiyo kuna hesabu za ma | Miaka mitatu si safari nyepesi, aghalabu inahusisha milima na mabonde, katika hiyo kuna hesabu za mafanikio na maanguko lukuki, ndivyo ilivyo hata katika utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya muda huo.
Rais Samia aliapishwa kuwa Rais, Machi 19, mwaka 2021 siku mbili baada ya kutangaza kifo cha aliyekuwa na wad... |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuja na Azimio la Mtwara, ikiwa ni hatua ba | Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuja na Azimio la Mtwara, ikiwa ni hatua baada ya kumalizika kwa maandamano yaliyofanyika katika Majiji manne nchini.
Kulingana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, msingi wa azimio hilo ni kutoa jawabu la nini kitafuata chenye sura ya mapambano baada ya... |
Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo (UKEF), imewatangazia fursa wafanyabiashara na waw | Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo (UKEF), imewatangazia fursa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania ya kuwadhamini katika taasisi za kifedha za kimataifa pale watakapohitaji mikopo.
Udhamini huo ni kwa wafanyabiashara wanaotarajia kukopa katika taasisi za fedha, lakini wamekosa dhamana zinazowa... |
Kama kuna changamoto kubwa na pengine wenye mamlaka ya kuchukua hatua hawana taarifa nayo, basi ni h | Kama kuna changamoto kubwa na pengine wenye mamlaka ya kuchukua hatua hawana taarifa nayo, basi ni hii ya huduma katika Vituo vya Afya na Zahanati nyakati za usiku.
Naeleza hili kwa sababu nimeshuhudia, wala sikuhadithiwa. Katika baadhi ya zahanati na vituo vya afya, huduma zinatolewa mchana pekee, nyakati za usiku ha... |
Safari ya miezi saba bila ya huduma ya nishati ya uhakika nchini imebakiza siku 18 kukoma rasmi, hii | Safari ya miezi saba bila ya huduma ya nishati ya uhakika nchini imebakiza siku 18 kukoma rasmi, hii ni baada ya matarajio ya kuingizwa kwa megawati 470 za umeme katika gridi ya taifa.
Megawati hizo zitatokana na umeme utakaozalishwa na mitambo miwili kati ya tisa ya mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) u... |
Takriban watu 25, wamepoteza maisha na wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mann | Takriban watu 25, wamepoteza maisha na wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne, likiwemo lori moja na mengine madogo matatu.
Idadi hiyo ya waliofariki imeongezeka kutoka vifo 15 vilivyoripotiwa juzi kutokana na ajali hiyo, iliyotokea katika eneo la Kibaoni, barabara kuu ya Arusha-Namanga mkoani ... |
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi amemshitaki Wakili wa Kujitegemea, Peter Madel | Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi amemshitaki Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kitaaluma.
Msingi wa tuhuma dhidi ya Madeleka kulingana na maelezo yake, ni hatua yake ya kumwakilisha mteja wake, Hashim Ally katika kesi iliyowahi kufunguliwa naye dhidi ya Mbunge... |
Serikali imetangaza mikakati ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa sukari, ikiwa ni hatua za kudu | Serikali imetangaza mikakati ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa sukari, ikiwa ni hatua za kudumu za kumaliza tatizo hilo ambalo aghalabu hujitokeza kila mwaka.
Ingawa si mara ya kwanza Serikali kuibuka na mikakati ya kumaliza tatizo hilo, lakini hii iliyotangazwa kwa mtazamo wangu naona uhai ndani yake.
Mikakat... |
Hatma ya kukoma kwa mgawo wa umeme nchini ipo ndani ya muda mchache, baada ya matarajio ya kuingizwa | Hatma ya kukoma kwa mgawo wa umeme nchini ipo ndani ya muda mchache, baada ya matarajio ya kuingizwa kwa megawati 235 katika gridi ya taifa.
Matumaini ya kukoma kwa mgawo huo, yanatokana na kile kilichoelezwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba kwamba muda wowote kuanzia sasa, mtambo kutoka Bwawa la Ji... |
Jukumu la uingizaji sukari kutoka nje ya nchi, halitakuwa tena mikononi mwa wazalishaji, baada ya Se | Jukumu la uingizaji sukari kutoka nje ya nchi, halitakuwa tena mikononi mwa wazalishaji, baada ya Serikali kutumia Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) kuingia mikataba na kampuni mbalimbali zitakazotekeleza wajibu huo.
Hatua hiyo itafuatiwa na mabadiliko ya sheria Juni mwaka huu, itakayowaondoa wazalishaji k... |
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametaka ukarabati wa miundombinu ya umeme kuf | Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametaka ukarabati wa miundombinu ya umeme kufanyika kwa wakati ili kuwaepusha wananchi na adha ya kukosa nishati hiyo kwa muda mrefu.
Maelekezo hayo ya Dk Biteko, yametokana na malalamiko yaliyoibuliwa na Mbunge wa Wanging’ombe, Dk Festo Dugange aliyelalamikia kuu... |
Shaka ya usalama imewagubika wakazi wa maeneo ya jirani na jengo la Motel Agip jijini Dar es Salaam, | Shaka ya usalama imewagubika wakazi wa maeneo ya jirani na jengo la Motel Agip jijini Dar es Salaam, wakihofu kuangukiwa na jengo hilo kutokana na kuchoka kwake.
Jengo hilo, kwa mujibu wa taarifa ilizonazo Mwananchi limejengwa tangu miaka ya 1940 na mwaka 1998 liliacha kutumika wala kufanyiwa matengenezo hadi sasa.
K... |
Siku ya kazi haikuwa kikwazo kwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Mkoa | Siku ya kazi haikuwa kikwazo kwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Mkoa wa Mbeya, kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho mkoani humo.
Maandamano hayo yamefanyika jana (Jumanne), siku ambayo kimsingi ni katikati ya wiki na isingetarajiwa umati huo kujitokeza ... |
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na maboresho yaliyofanywa katika bandari y | Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na maboresho yaliyofanywa katika bandari ya Dar es Salaam, kuna haja ya kuongezwa gati namba 13 hadi 15 ili kuongeza ufanisi wa bandari hiyo.
Katika kufanikisha kazi hiyo, Profesa Mbarawa amezikaribisha kampuni za uwekezaji kutoka Misri kushirikiana na Tanzania... |
Kama ulidhani kupaa kwa bei ya bidhaa kumeishia kwenye sukari pekee mambo ni tofauti, hali hiyo imeb | Kama ulidhani kupaa kwa bei ya bidhaa kumeishia kwenye sukari pekee mambo ni tofauti, hali hiyo imebainika hata katika bidhaa nyingine za nafaka, vikiwemo viazi, vitunguu na pilipili hoho.
Kuongezeka kwa bei ya bidhaa hizo, kunazusha hofu kwa waumini wa dini ya kiislamu ambao Machi 10 au 11, mwaka huu wanatarajia kuan... |
Mambo matatu yamebainika kuwa chanzo cha bei ya sukari kuendelea kupaa, licha ya Serikali kuagiza ta | Mambo matatu yamebainika kuwa chanzo cha bei ya sukari kuendelea kupaa, licha ya Serikali kuagiza tani 50,000 nje ya nchi na kupanga bei elekezi ya bidhaa hiyo.
Mambo hayo ni changamoto katika utaratibu wa usambazaji, mahitaji makubwa yanayozidi sukari iliyoagizwa na janja janja za wauzaji wa rejareja.
Sababu hizo zi... |
Safari ya mwisho wa maisha ya duniani ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa itakamilikia kijijini k | Safari ya mwisho wa maisha ya duniani ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa itakamilikia kijijini kwao Ngarash, Monduli mkoani Arusha.
Katika kijiji hicho, ndiko mwanasiasa huyo aliyewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali serikalini atazikwa Februari 17, mwaka huu.
Lowassa aliaga dunia Februari 10, mwaka huu katika ... |
Kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi na mapenzi, mabadiliko ya utendaji wa Jeshi la Polisi na kudumishwa | Kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi na mapenzi, mabadiliko ya utendaji wa Jeshi la Polisi na kudumishwa kwa utawala wa sheria ni miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa na viongozi wa dini kama suluhu ya matukio ya kutoweka kwa watu.
Mengine yaliyoonekana kuleta jawabu la matukio hayo, kwa mujibu wa viongozi hao wa dini ni k... |
Takriban Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni), zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ma | Takriban Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni), zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya Reli ya Tanzania-Zambia, yenye umri wa karibu miongo mitano sasa.
Taarifa kuhusu gharama za maboresho ya reli hiyo, imetolewa na taifa la China, kupitia balozi anayeliwakilisha taifa hilo nchini Zambia, Du ... |
Kutokana na wizi wa transfoma 85 uliofanyika katika kipindi cha Januari mwaka huu, Shirika la Umeme | Kutokana na wizi wa transfoma 85 uliofanyika katika kipindi cha Januari mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema thamani ya hasara iliyopatikana kutokana na wizi huo ni takriban Sh500 milioni.
Taarifa kuhusu wizi wa transfoma hizo, iliwekwa wazi bungeni jijini Dodoma juzi na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia... |
Kutokana na msongamano wa malori yanayosubiri kushusha Kopa katika bandari kavu, Bandari ya Dar es S | Kutokana na msongamano wa malori yanayosubiri kushusha Kopa katika bandari kavu, Bandari ya Dar es Salaam imepanga kuitumia bandari kavu ya Kwala kuwa kituo cha kushushia mizigo yote ya madini hayo.
Kitakachofanyika kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho ni malori yote kupeleka mzigo huo K... |
Bandari ya Dar es Salaam imepanga kupitisha mizigo yote ya Kopa katika bandari kavu ya Kwala mkoani | Bandari ya Dar es Salaam imepanga kupitisha mizigo yote ya Kopa katika bandari kavu ya Kwala mkoani Pwani kabla ya kufikishwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirishwa.
Hatua hiyo, inalenga kupunguza msongamano wa malori katika bandari kavu inayotumika sasa iliyopo Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.
... |
Licha ya ugonjwa wa macho mekundu 'Red Eyes' ulioibuka nchini Tanzania kuwa tishio kwa wakazi wa nch | Licha ya ugonjwa wa macho mekundu 'Red Eyes' ulioibuka nchini Tanzania kuwa tishio kwa wakazi wa nchi hiyo, wapo wanaofaidika kutokana na kuwepo kwake.
Ugonjwa huo ulioripuka tangu wiki tatu zilizopita, kwa mujibu wa mamlaka za Tanzania takriban Mikoa 17 ya taifa hilo la Afrika Mashariki inataabika nao.
Wizara ya Afy... |
Kutoka kuwa na nchi wanachama 15 wa sasa, huenda Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Magharibi (Ecow | Kutoka kuwa na nchi wanachama 15 wa sasa, huenda Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) ukabaki na wanachama 12 pekee.
Hatua hiyo itafikiwa iwapo juhudi za mazungumzo hazitafua dafu kuhakikisha jumuiya hiyo inasalia na idadi ya siku zote ya wanachama wake.
Hofu ya Ecowas kupoteza wanachama wake watatu... |
Jeshi la Uhamiaji limesema hatua yake ya kumkamaka mwanaharakati, Mdude Nyangali katika mpaka wa Nam | Jeshi la Uhamiaji limesema hatua yake ya kumkamaka mwanaharakati, Mdude Nyangali katika mpaka wa Namanga akielekea nchini Kenya, imetokana na maelekezo kutoka Jeshi la Polisi.
Taarifa za kukamatwa kwa mwanaharakati huyo, zilisambaa kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), zikichapishwa na Wakili Peter Madeleka.
Katika ... |
Baada ya ahadi kadhaa za utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Mbamba Bay, hatimaye mradi huo upo mbion | Baada ya ahadi kadhaa za utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Mbamba Bay, hatimaye mradi huo upo mbioni kuanza kutekelezwa.
Awali Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliahidi kuanza utekelezaji huo Januari mwaka jana, baadaye Machi ilielezwa Sh70 bilioni zimeshatolewa na Serikali kuianza kazi hiyo.
Hatimaye... |
Rais Samia Suluhu Hassan ameweka dhamira ya kuvutia uwekezaji wa Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi y | Rais Samia Suluhu Hassan ameweka dhamira ya kuvutia uwekezaji wa Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni) kutoka nchini Indonesia, huku akitaja sababu tano za kwanini Tanzania ni eneo sahihi la kuwekeza.
Jukumu la kufanikisha upatikanaji wa uwekezaji huo, amelitoa kwa taasisi za Serikali, alipozungumza na ... |
Safari ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai haki kwa njia ya maandamano ndiyo imeanz | Safari ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai haki kwa njia ya maandamano ndiyo imeanza, huku Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akisisitiza kuendelea kufanya hivyo katika Mikoa mbalimbali hadi Serikali itakapowaelewa.
Msingi wa maandamano ya chama hicho ni kuishinikiza Serikali itekeleze mambo man... |
Bandari ya Tanga inatarajiwa kuwa na uwezo wa kupokea tani milioni 3 za mizigo kwa mwaka, hatua itak | Bandari ya Tanga inatarajiwa kuwa na uwezo wa kupokea tani milioni 3 za mizigo kwa mwaka, hatua itakayofikiwa kutokana na maboresho ya miundombinu mbalimbali katika bandari hiyo.
Kutokana na miundombinu iliyopo sasa, bandari hiyo ina uwezo wa kupokea tani 750,000 kwa mwaka.
Akizungumza mkoani Tanga, Meneja wa bandari... |
Miongoni mwa malalamiko makubwa ya wananchi katika Mikoa mbalimbali nchini kwa sasa ni kuongezeka kw | Miongoni mwa malalamiko makubwa ya wananchi katika Mikoa mbalimbali nchini kwa sasa ni kuongezeka kwa bei ya sukari kutoka Sh2,500 na Sh3,000 hadi Sh5,000.
Ongezeko hilo la bei hiyo limetokana na uhaba wa bidhaa hiyo madukani, unaosababishwa na kupungua kwa uzalishaji wa sukari viwandani.
Kupungua huko kwa uzalishaji... |
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na m | Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na mabadiliko ya taasisi za familia.
Hali hiyo, alisema inaibua haja ya kila anayepaswa kulinda taasisi hiyo kujitathmini juu ya wajibu wake
Rais Samia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipohutubia katika hafl... |
Licha ya miezi sita iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) | Licha ya miezi sita iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumaliza mgao wa umeme nchini kukaribia ukingoni, bado kuna mashaka ya mgawo huo kumalizika.
Septemba 26, mwaka jana, wakati akimuapisha bosi mpya wa Tanesco, Rais Samia alilitaka shirika hilo kuhakikisha linamaliza mga... |
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na m | Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na mabadiliko ya taasisi za familia.
Hali hiyo, alisema inaibua haja ya kila anayepaswa kulinda taasisi hiyo kujitathmini juu ya wajibu wake
Rais Samia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipohutubia katika hafl... |
Mambo bado magumu kwa chama cha siasa tarajiwa cha IPP kuhusu kupata usajili wa muda, kikieleza kuum | Mambo bado magumu kwa chama cha siasa tarajiwa cha IPP kuhusu kupata usajili wa muda, kikieleza kuumiza na ucheleweshwaji wa usajili wake unaofanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, huku ofisi hiyo ikitaja kutokidhi masharti ndiyo sababu ya yote.
Malalamiko ya chama hicho tarajiwa juu ya kucheleweshewa usajili ... |
Serikali imeanza kuwapika mawakili wake kwa kuwajengea uwezo wa kuzikabili kesi zitakazojitokeza baa | Serikali imeanza kuwapika mawakili wake kwa kuwajengea uwezo wa kuzikabili kesi zitakazojitokeza baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mafunzo kwa mawakili hao yanatokana na kile kilichoelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi kuwa, kuna matarajio ya mabadi... |
Wafanyabiashara wadogo sita walioathiriwa na maporomoko ya tope wilayani Hanang mkoani Manyara, wame | Wafanyabiashara wadogo sita walioathiriwa na maporomoko ya tope wilayani Hanang mkoani Manyara, wamesamehewa deni la Sh22 milioni walilotakiwa kurejesha kwa kipindi cha miezi mitatu.
Fedha hizo walikuwa wanadaiwa na Taasisi ya kifedha ya VisionFund Tanzania na Metro Life Assurance, walizozikopa kwa shughuli za biashar... |
Safari ya kuifikisha Tanzania katika matumaini ya uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme si hadi | Safari ya kuifikisha Tanzania katika matumaini ya uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme si hadithi tena, bali ni jambo lenye uhalisia.
Kinachoubeba uhalisia huo ni kile kinachoshuhudiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati hasa Mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).
Ulianza kama hadit... |
Ukiingia ‘Gesti’ huwa unaandika jina lako halisi? Swali hili linaakisi tabia ya wateja wengi wa nyum | Ukiingia ‘Gesti’ huwa unaandika jina lako halisi? Swali hili linaakisi tabia ya wateja wengi wa nyumba za kulala wageni, ambao aghalabu hutumia majina bandia kuandika katika vitabu vya wageni.
Achana na hoteli ambazo kwa kawaida huwa na utaratibu unaolazimu kuchukua taarifa za mteja kabla ya kuingia, wakati mwingine h... |
Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumteuwa Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu wake Mkuu, wanasiasa wa | Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumteuwa Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu wake Mkuu, wanasiasa wa chama hicho wamesifu uteuzi wake, huku wapinzani wakimtahadharisha na siasa za mabavu.
Dk Nchimbi ameteuliwa leo Januari 15, 2024 na Kamati Kuu ya CCM na baadaye kuridhiwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho, iliyoketi v... |
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimempitisha Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichuk | Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimempitisha Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, mwaka jana.
Kujiuzulu kwa Chongolo, kulitokana na kile alichoandika katika barua yake Novemba 27 mwaka jana kuwa, amelazimika kuwajibika kutokana na ... |
Nchi zilizoendelea zinatarajiwa kukumbwa na athari ya asilimia 60 katika ajira zake, kutokana na kui | Nchi zilizoendelea zinatarajiwa kukumbwa na athari ya asilimia 60 katika ajira zake, kutokana na kuingia kwa teknolojia ya akili bandia (AI).
Hayo yameelezwa leo Jumatatu, Januari 15, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Kristalina Georgieva alipozungumza katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Dunian... |
Huenda leo swali kuhusu mrithi wa Daniel Chongolo katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduz | Huenda leo swali kuhusu mrithi wa Daniel Chongolo katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) likapata majibu, hii inatokana na kufanyika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho.
Kikao hicho kinachofanyika visiwani Zanzibar leo Jumatatu, Januari 15, 2024 kikiongozwa na Mwenyekiti wa CC... |
Ili kuongeza tija ya ushirikiano baina ya Tanzania na Angola, mataifa hayo yamekutana kujadili masua | Ili kuongeza tija ya ushirikiano baina ya Tanzania na Angola, mataifa hayo yamekutana kujadili masuala ya kisiasa, diplomasia, ulinzi na usalama.
Mkutano huo wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPU), umeanza kufanyika leo, Januari 14 hadi 16, mwaka 2024, ukihusisha ngazi ya maofisa waandamizi wa Serikali na Mawaziri.
H... |
Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na uny | Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na unyanyasaji wa kingono katika vyombo vya habari.
Hayo ni kulingana na utafiti wa hali ya usalama wa wanahabari wanawake katika vyumba vya habari uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika vyombo vy... |
Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na uj | Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na ujuzi na maarifa muhimu ili kujenga ustawi wa karne ya 21.
Kwa kutambua hitaji hilo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua mpango wa kuanzisha klabu za kidigitali, unaolenga kukuza ujuzi wa kidijitali na ubunif... |
Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Romania, Klaus Iohannis atakayewasili nchini kesho kwa | Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Romania, Klaus Iohannis atakayewasili nchini kesho kwa ziara ya kitaifa ya siku nne.
Ziara ya mkuu huyo wa taifa hilo la Ulaya, inatazamwa kama tumaini jipya la kufufuka kwa biashara kati ya Tanzania na Romania iliyoshuhudiwa ikidorora kwa miaka ya hivi karibuni.
Hilo linath... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.